Un Staff Officer Course
Kozi ya Unadhimu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2023
Muda wa kozi: Wiki nne
Ada kwa ajili ya kozi: Kozi inadhaminiwa na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)
Vigezo na Mashart
Malazi na chakula kwa washiriki wa kozi hiyo yatatolewa na JWTZ (Kozi itadhaminiwa na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa)
Utangulizi
Kutokana na kuongezeka kwa migogoro ambayo husababisha ukosefu wa usalama na amani Umoja wa Mataifa ulianzisha namna mbalimbali za kulinda amani.
Due to the growing number of complex crises that pose threats to international peace and security the United Nations introduced a multi-dimensional approach to peacekeeping. Kutokana na changamoto za utendajikazi kwa Maafisa Wanadhimu hususani wanajeshi katika ngazi ya mbalimbali za Makao Makuu, JWTZ limeweza kukabiliana na upungufu wa Maafisa wanadhimu kwa kuendesha mafunzo mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ili kufikia viwango vinavyohitajika katika utekelezaji wa majukumu yao katika ngazi za kioperesheni na stratejia.
Kwa sasa Kituo cha Mfunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania kimeweza kuendesha awamu 12 za Mafunzo kwa Maafisa Wanadhimu wa Umoja wa Mataifa ili kuwajengea uwezo na maarifa yatakayo saidia katika kutekeleza jukumu la ulinzi wa amani
Maelezo ya Kozi
Kozi ya Unadhimu wa Umoja wa Mataifa inalenga kuwapa washiriki wa kozi hiyo ujuzi , uzoefu na mazoezi yanayohusiana na majukumu ya Maafisa Wanadhimu wanapokuwa katika ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali.
Moduli za kozi
Mafunzo ya kozi hii yanalenga kufanikisha wigo wa mafunzo yanayotolewa na kitengo cha Ulinzi wa amani na utendaji kivita cha Umoja wa Mataifa. Mafunzo hayo yatahusisha mafunzo maalum ya umoja huo. Vile vile mwisho wa mafunzo ya kozi hiyo kutakuwa na mazoezi mbalimbali.
Washiriki wa kozi
Walengwa wa kozi hiyo ni Maafisa ngazi ya kati na juu ya uongozi katika JWTZS
Maelezo ya kozi |
|
Muda wa kozi |
wiki nne |
Idadi ya washiriki |
Maafisav 35 |
Walengwa |
Maafisa wa JWTZ |
Lugha inayotumika kufundishia |
Kiingereza |